Na mwandishi wetu
Bondia wa ngumi za kulipwa Twaha Kassim ‘Kiduku’ anatarajiwa kurejea ulingoni Septemba 3 mwaka huu dhidi ya mpinzani ambaye atatangazwa baadaye ikiwa ni baada ya kukaa tarkiban miezi minne bila pambano.
Mara ya mwisho Kiduku alipanda ulingoni Machi 26, mwaka huu dhidi ya bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Alex Kabangu, pambano aliloshinda na kubeba mkanda wa kimataifa wa UBO, katika pambano la uzito wa kati lililofanyika Morogoro.
Mratibu wa mapambano ya ngumi, Seleman Semenyu alisema pambano la Kiduku liko njiani na huenda likafanyika mikoani hasa mkoani Morogoro kama atapata mdhamini atakayetoa kuanzia Sh 30 milioni.
“Nashukuru kwa kumaliza pambano la Selemani Kidunda dhidi ya Erick Katompa salama, na sasa bado kazi ipo mbele, tunaelekea kuandaa pambano kubwa la Kiduku, linaweza kupelekwa mikoani kama tukipata wadhamini wa kutuwezesha,” alisema Semunyu.
Kwa miaka ya karibuni Kiduku mzaliwa wa Morogoro amekuwa katika kiwango bora na kuendelea kuweka heshima ya jina lake na taifa. Kwenye mapambano kadhaa aliyocheza katika ardhi ya nyumbani amekuwa bora zaidi kuliko yale anayoenda kucheza anga la kimataifa.
Takwimu za mtandao wa ngumi wa Boxrec zinaonesha Kiduku anayeshika nafasi ya kwanza Tanzania kwa ubora katika uzito wa Super Middle, amecheza jumla ya mapambano 28 akiwa ameshinda 19, sare nane na kupoteza mmoja.
Ngumi Kiduku aandaliwa pambano
Kiduku aandaliwa pambano
Read also