Na mwandishi wetu
Kocha wa Mbeya Kwanza, Mbwana Makata amefungiwa kushiriki mchezo wa soka kwa kipindi cha miaka mitano kwa kosa la kushawishi wachezaji wasiingie uwanjani kuanza mchezo wao dhidi ya Namungo uliokuwa upigwe Uwanja wa Ilulu, Lindi mnamo Aprili 13, mwaka huu.
Maamuzi hayo yametolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi wa Bodi ya Ligi Kuu ikiwa ni pamoja na kuipa ushindi wa mabao matatu na pointi tatu timu ya Namungo kama matokeo ya mchezo huo.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa Makata ambaye ni kipa wa zamani wa Yanga, aliwashawishi wachezaji hao wasiingie uwanjani kucheza mechi hiyo kwa madai kuwa gari la wagonjwa (ambulance) lilichelewa kufika uwanjani hapo wakati ni kinyume na ilivyokuwa kulingana na kanuni ya muda wa kuchelewa kufanyika kwa mchezo.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 17:42 ya Ligi Kuu, mchezo unaweza kuchelewa kuanza kwa hadi dakika 30 kama timu itachelewa kufika uwanjani au kutotimizwa kwa taratibu za msingi za mchezo na baada ya muda huo kamishna wa mchezo anaweza kuamua mchezo uvunjwe.
Mbali na Makata, mwingine aliyepewa adhabu hiyo ni Meneja wa Mbeya Kwanza, David Naftali. Adhabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 32:7 ya Ligi Kuu kuhusu kuvuruga mchezo.
Soka Mbwana Makata afungiwa miaka mitano
Mbwana Makata afungiwa miaka mitano
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
