Na mwandishi wetu
Simba SC inatarajia kuwafahamu wapinzani wao Jumamosi hii kwenye michuano mipya ya African Football League (AFL) katika droo itakayochezeshwa mjini Cairo, Misri.
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) mbali na kutaja tarehe ya droo hiyo lakini pia iliweka wazi ratiba ya michuano hiyo itakayoshirikisha timu nane kabla ya msimu ujao kujumuisha timu 24 za juu Afrika.
Mechi za robo fainali za michuano hiyo zitaanza kuunguruma Oktoba 20 ambapo nusu fainali itachezwa Oktoba 29 na Novemba Mosi kabla ya mechi za fainali itakayopigwa Novemba 5 na 11, mwaka huu.
“Toleo hili la kihistoria la uzinduzi wa AFL litafanyika kwa muda wa wiki nne, sherehe za ufunguzi na mechi ya kwanza itafanyika Oktoba 20 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Nusu fainali itafanyika kati ya Oktoba 29 na Novemba Mosi na fainali ambazo zitaamua mshindi wa kwanza zitafanyika Novemba 5 na 11, mwaka huu,” ilieleleza taarifa ya Caf.
Ukiachana na Simba inayoiwaikilisha Tanzania, timu nyingine zitakazoshiriki msimu huu ni Al Ahly ya Misri, Enyimba (Nigeria), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Petro Atletico (Angola), TP Mazembe (DR Congo) na Wydad AC (Morocco).
Kimataifa Wapinzani wa Simba AFL kujulikana Jumamosi
Wapinzani wa Simba AFL kujulikana Jumamosi
Read also