Juventus, Italia
Kiungo wa Juventus na timu ya Taifa ya Ufaransa, Paul Pogba amejibu vitisho vilivyoelekezwa kwake na kaka yake Mathias Pogba ambaye amepanga kuanika kila kitu kuhusu maisha ya soka ya mchezaji huyo.
Mathias ambaye amecheza soka katika nchi mbalimbali lakini kwa sasa hana klabu anayoichezea, ametupia video kupitia mtandao wa Instagram akitoa vitisho hivyo dhidi ya ndugu yake ambapo ameahidi kufunguka makubwa kuhusu Paul Pogba na mwanasheria na wakala wa mchezaji huyo, Rafaela Pimenta.
Mathias mbali na Pogba pia ameahidi kufunguka makubwa kuhusu mshambuliaji wa Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, Kylian Mbappe ambaye kama Pogba wote pia wanaichezea timu ya Taifa ya Ufaransa.
Akijibu shutuma na vitisho hivyo, Pogba alisema, “kusudio la hivi karibuni kutoka kwa Mathias Pogba kupitia mitandao ya kijamii kwa bahati mbaya si kitu cha kushangaza, ni dhamira ambayo imekuja baada ya vitisho vya kutaka mali vilivyoandaliwa na genge lililojipanga dhidi ya Paul Pogba, yote haya tayari nimeyaripoti kwenye mamlaka husika za Italia na Ufaransa mwezi mmoja uliopita.”
Habari za ndani zinadai kwamba uchunguzi unaendelea kuhusu vitisho hivyo dhidi ya Pogba, vitisho ambavyo vinatajwa kuwa si vya kupuuzia
Mathias mwenye umri wa miaka 32, kwa sasa hana timu baada ya kuachana na klabu ya Ligi Daraja la Nne nchini Ufaransa ya Belfort, Aprili mwaka huu ingawa amewahi kucheza soka katika klabu kadhaa za barani Ulaya.
“Dunia nzima inatakiwa kufahamu baadhi ya mambo ili umma uamue kama Paul ni kweli ana hadhi na heshima na vipi nafasi yake kwenye timu ya Taifa ya Ufaransa, kama kweli ni mtu muaminifu na ana hadhi ya kuwawakilisha vijana duniani, au makampuni makubwa,” alisema Mathias katika madai aliyoyatoa mitandaoni Jumamosi.
Mathias pia alitoa shutuma na kuhoji hadhi na utendaji kazi wa kiweledi wa Pimenta ambaye alisema ndugu yake Paul anamchukulia kama ndiye mama yake wa pili.
Kimataifa Pogba, kaka yake waingia vitani
Pogba, kaka yake waingia vitani
Read also