Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma amesema timu yake itamaliza msimu kwenye nafasi nne za juu kutokana na kiwango walichokuwa nacho na idadi ya mechi zilizobaki.
Juzi mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu (daraja la kwanza) waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu FC wakiwa uwanja wao wa nyumbani, CCM Mkwakwani na kurudi nafasi ya nne kwa kufikisha pointi 30.
“Naridhishwa sana na kiwango tunachokionesha, wachezaji wangu wamekuwa wasikivu sana kwa kufuata kile ninachowaelekeza, tupo nafasi ya nne na ninaamini tutaipigania hadi mwisho,” alisema Ouma.
Kocha huyo alisema mikakati yao kwa sasa ni kuhakikisha wanashinda mechi zao tisa zilizobaki ili kufikia kwa vitendo kile ambacho wamekikusudia cha kushiriki michuano ya kimataifa.
Coastal ambao ni mabingwa wa taji la ligi kuu mwaka 1988 (wakati huo ligi daraja la kwanza) wamesema endapo lengo lao la kushiriki michuano ya kimataifa litatimia msimu ujao wataimarisha kikosi kwa ajili ya kuwania taji la Ligi Kuu NBC.
Soka Ouma aiweka Coastal top four
Ouma aiweka Coastal top four
Read also