Barcelona, Hispania
Rais wa klabu ya Barcelona, Joan Laporta ameshitakiwa kwa makosa ya rushwa yanayohusisha malipo yaliyofanywa katika kampuni zinazohusishwa na aliyekuwa makamu rais wa kamati ya waamuzi Hispania, Jose Maria Negreira.
Makosa hayo yanahusisha matukio ya miaka ya nyuma wakati Laporta (pichani juu) akiwa kiongozi wa klabu hiyo kati ya mwaka 2003 na 2010.
Laporta ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Barcelona kwa mara nyingine mwaka 2021, pamoja naye watuhumiwa wengine ni marais wa zamani wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu na Sandro Rosell pamoja na mtoto wa Negreira aitwaye, Javier Enriquez Romero.
Jaji anayesimamia kesi hiyo pia alisema kwamba wajumbe wote wa bodi waliokuwapo wakati malipo hayo yakifanyika nao waingizwe katika kesi hiyo.
Klabu ya Barcelona au Barça inadaiwa kumlipa Negreira Dola 7.3 milioni kati ya mwaka 2001 na 2018 kupitia kampuni yake na wakati malipo hayo yakifanyika Negreira alikuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Hispania.
Akijitetea Laporta alisema kwamba malipo hayo yalifanyika kwa ajili ya kuandaliwa ripoti ya video ya ufundi inayohusu namna waamuzi wanavyochezesha mechi za timu hiyo na si kwa ajili ya ushawishi wa kuwataka waamuzi waipendelee timu yao.
Kimataifa Rais Barca ashitakiwa kwa rushwa
Rais Barca ashitakiwa kwa rushwa
Read also
