Na mwandishi wetu
Bondia wa ngumi za kulipwa, Seleman Kidunda amewahimiza mashabiki kufika kwa wingi kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma kumshuhudia akiwawakilisha vyema na kumaliza utata kwenye pambano lake dhidi ya Tshimanga Katompa raia wa DR Congo.
Pambano hilo lililopewa jina la Payback Night linatarajiwa kupigwa Julai 30, mwaka huu likiwa ni la kuwania ubingwa wa dunia wa Shirikisho la Kimataifa la Ngumi (WBF) na litapiganwa kwa raundi 10.
Pambano hilo linanogeswhwa na upinzani wa wawili hao wanapokutana kwani katika pambano lao mara ya mwisho walipigana Desemba 26 mwaka jana na Kidunda aliibuka kidedea kwa ushindi wa TKO na kuweka rekodi ya kushinda mapambano saba kwa KO.
“Nahitaji sapoti ya Watanzania, wakazi wa Songea hii ni zamu yao kuja kuona kazi yangu, mashabiki na wadau wengi wa ngumi wanataka kujua nani mbabe kati yangu na Katompa sasa niwaambie tu waje kushuhudia wenyewe kwa macho yao,” alisema Kidunda maarufu kama Mtu Kazi Mtu Chuma.
Kwa upande wake promota wa pambano hilo, Selemani Semunyu amesema kwamba pambano hilo pia litasindikizwa na mapambano mengine ya utangulizi kutoka kwa mabondia bora watakaonogesha ndondi za siku hiyo.
Ngumi Kidunda awaita mashabiki Majimaji
Kidunda awaita mashabiki Majimaji
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
