London, England
Wimbi jipya la virusi vya omicron vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19 limeibua hofu katika Ligi Kuu England hali iliyosababisha baadhi ya mechi za ligi hiyo kuahirishwa.
Mechi ya Man United na Brentford imeahirishwa kutokana na hofu ya maradhi hayo kama ilivyo kwa mechi kati ya Tottenham na Brighton pamoja na ile ya Burnley na Watford ambayo ilikuwa ipigwe Jumatano nayo imeahirishwa.
Kutokana na hofu hiyo, kocha wa Brentford, Thomas Frank ameshauri ligi hiyo kusimamishwa baada ya watu 13 katika timu yake baadhi wakiwa wachezaji kupimwa na kukutwa na virusi vya maradhi hayo.
Kwa upande wa Man United, mara baada ya ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Norwich Jumamosi iliyopita, vipimo vilifanywa kwa wachezaji na maofisa wa klabu hiyo na watu 42 wakakutwa wameathirika na virusi hivyo ingawa ripoti hiyo haikubainisha wachezaji ni wangapi.
Tayari mechi ya jioni hii kati ya Leicester na Tottenham imeahirishwa lakini haikuweza kufahamika haraka iwapo mechi nyingine za jioni hii kati ya Chelsea na Everton na Liverpool na Newcastle kama nazo zitaahirishwa.
Kuibuka kwa kirusi cha Omicron kumeibua hali ya wasiwasi katika nchi mbalimbali ikiwamo Uingereza na hivyo haitoshangaza kuanza kutolewa maelekezo au amri kuwataka watu kutumia barakoa na kuepuka mikusanyiko isiyo lazima.
Kimataifa Corona yazua hofu EPL
Corona yazua hofu EPL
Related posts
Read also