Na mwandishi wetu
Matarajio ya Simba kutoka na pointi tatu katika mechi yake ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Pamba Jiji yamekwama baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
Matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi Machi 19, 2026 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza yamewakera mashabiki wa Simba waliojipa matumaini ya kubeba pointi tatu hasa baada ya hasimu wao Yanga kutoka sare ya bao 0-0 na TRA United.
Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuzichana nyavu za Pamba katika dakika ya 32 kwa bao lililofungwa na Anicet Oura lakini shuti la mbali lililopigwa na James Mwashenga dakika tatu baadaye lilitosha kuipa Pamba bao la kusawazisha.
Kwa matokeo hayo, Simba ambao hadi sasa wamecheza mechi 13 wamefikisha pointi 28 na kutulia nafasi ya tatu wakiachwa kwa tofauti ya pointi tisa na mahasimu wao Yanga wanaoshika usukani wa ligi hiyo wakiwa wamecheza mechi 15.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Mashujaa FC waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Lake Tanganyika kulazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC.
Soka Pamba yaibana mbavu Simba
Pamba yaibana mbavu Simba
Read also
