Na mwandishi wetu
Azam FC imenyakua pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa Jumatano Aprili 1, 2026 kwenye Uwanja wa Airtel mjini Singda.
Kipigo hicho ni mwendelezo wa matokeo yasiyopendeza kwa Singida Black ambayo ni hivi karibuni tu imetoka kuchezea kichapo kingine cha mabao 3-0 mbele ya Yanga na hivyo kubakiwa na pointi 25 katika mechi 16.
Kwa upande wa Azam ushindi huo umeendelea kufufua matumaini ya timu hiyo kwenye mbio za kulisaka taji la ligi ikiwa imefikisha pointi 32 katika mechi 16 na kuwasogelea vinara Yanga kwa tofauti ya pointi sita.
Azam ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 50 mfungaji akiwa ni Lusajo Mwaikenda baada ya kuiwahi krosi iliyochongwa na Idd Suleiman ‘Nado’ ambaye pia alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Dakika 15 baadaye, Azam waliandika bao la pili lililofungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye aliuwahi mpira akiwa ndani ya eneo la penalti na kupiga shuti dhaifu lililojaa wavuni.
Singida walipambana na katika dakika ya 70 walifanikiwa kupata bao pekee lililofungwa na Lyanga, bao lililotokana na mpira wa adhabu iliyopigwa na Ande Koffi.
Soka Azam yaiadhibu Singida Black
Azam yaiadhibu Singida Black
Read also
