Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Barcelona, Pierre-Emerick Aubameyang amevamiwa nyumbani kwake na kupigwa na majambazi waliokuwa na silaha mbalimbali zikiwamo za chuma.
Klabu ya Barcelona imethibitisha kutokea kwa uvamizi huo Jumatatu hii ambapo Aubameyang na mkewe walifungwa pingu kwa muda wa tukio hilo ingawa hakuna kati yao aliyeachwa na majeraha makubwa.
Mapema Jumatatu hii, majambazi hao walivunja na kuingia nyumbani kwa mwanasoka huyo anayeishi na mkewe na watoto wake wawili jijini Barcelona kwenye nyumba ambayo ipo umbali wa mita 200 kutoka katika nyumba ambazo bado zinamilikiwa na mastaa wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi na Luis Suarez ambao makazi yao yanalindwa na kampuni maalum za ulinzi.
Aubameyang alikuwa ndio kwanza amerudi nyumbani kwake baada ya Jumapili timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Real Valladolid katika mechi ya La Liga, mechi ambayo mchezaji huyo alikaa benchi.
Kwa mujibu wa habari za ndani, majambazi hao wanadaiwa kumlazimisha mchezaji huyu kufungua kabati ambalo lilikuwa na vito mbalimbali vya thamani ambavyo ni kati ya vitu walivyoondoka navyo na hakuna mtu aliyekamatwa wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.
Aubameyang amevamiwa ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Robert Lewandowski kuporwa saa wakati akiingia mazoezini. Saa hiyo iliyoporwa kwenye gari la mchezaji huyo thamani yake inadaiwa kufikia Euro 70,000.
Kimataifa Aubameyang avamiwa, afungwa pingu
Aubameyang avamiwa, afungwa pingu
Read also