Na mwandishi wetu
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana amesema ubalozi uko tayari kuipokea na kuipa sapoti timu ya taifa ya Wanawake, ‘Twiga Stars’ inayotarajia kuivaa Banyana Banyana kuwania kufuzu Michezo ya Olimpiki.
Mchezo huo ambao ni wa marejeano unatarajia kuchezwa Februari 27 mwaka huu huko Mbombela, Nelspruit nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania, balozi huyo alisema wao kama ubalozi wamejiandaa na mapokezi hayo na wana furaha kwa kuwa Twiga itakwenda kucheza mchezo muhimu.
“Tuna uhakika Watanzania watajitokeza kwa wingi kuwashangilia wachezaji wetu wa Twiga Stars ambao wanakuja kuiwakilisha nchi kwenye mchezo huu mkubwa na muhimu.
“Tunalazimika kushinda na sisi kama balozi tutajitahidi kuwahamasisha na kuwapa ulinzi wa kutosha wachezaji wetu ili kupata matokeo mazuri,” alisema Balozi Bwana.
Kiongozi huyo anayehudumu pia katika nchi za Botswana na Lesotho, amewaomba Watanzania kuiombea ushindi timu ya Twiga Stars ili ifanye vizuri kwenye mechi hiyo ambayo ni muhimu.
Kimataifa Balozi awaita Twiga Stars Afrika Kusini
Balozi awaita Twiga Stars Afrika Kusini
Read also