Na mwandishi wetu
Mwamuzi wa zamani wa Fifa ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Soka Tanzania (Frat) na mkufunzi wa waamuzi Tanzania, Omar Abdulkadir amefariki dunia leo Ijumaa.
Kufuatia kifo hicho Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walace Karia ametuma salamu za pole kwa Frat, ndugu, jamaa na wanafamilia wa mpira na wote walioguswa na msiba huo.
Taarifa ya TFF iliyopatikana kwenye vyanzo mbalimbali vya shirikisho hilo na kusainiwa na ofisa habari wake, Cliford Ndimbo ilimtaja marehemu kuwa ni mtu ambaye ataendelea kukumbukwa daima kwa mchango wake katika maendeleo ya mpira hasa eneo la waamuzi.
Nayo klabu ya Simba katika salamu zake za pole ilimuelezea marehemu kwa namna ambavyo alikuwa mwamuzi mahiri kabla ya kustaafu akiwa mwamuzi mwenye beji ya Fifa.
Wakati wa uhai wake, Abdulkadir alijijengea heshima na umaarufu kutokana na umakini wake wa kusimamia mechi jambo ambalo lilimuwezesha kuwa miongoni mwa waamuzi wachache wa miaka ya nyuma kuwa na beji ya Fifa.
Soka Mwamuzi Omar Abdulkadir afariki
Mwamuzi Omar Abdulkadir afariki
Related posts
Read also
