Na mwandishi wetu
Baada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na timu ya KMC, mshambuliaji Shaban Chilunda amesema bao hilo litamuongezea ari ya kuendelea kupambana na kufunga mechi zijazo.
Chilunda ambaye alifunga bao hilo kwenye sare ya 1-1 dhidi ya JKT Tanzania, alisema kwamba bao hilo limefufua pia matumaini ya kuendelea kung’ara akiwa na uzi wa KMC msimu huu.
“Naamini kocha ataendelea kunipa nafasi ili niendeleze hiki ambacho nimekianza, kwa muda mrefu nilikuwa nalisaka bao hili na najisikia furaha kulipata sababu litaniongezea ari ya kujiamini,” alisema Chilunda.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kucheza soka la kulipwa CD Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza Hispania, alisema kwa sapoti anayoipata akiwa na timu hiyo anaamini atarudi kwenye kiwango chake na kuisaidia timu hiyo kufikia malengo.
Chilunda ni miongoni mwa wachezaji walioibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha Akademi ya Azam FC na kupandishwa timu ya wakubwa na baadaye kuuzwa Tenerife kabla ya kutua Simba na sasa KMC.
Soka Bao lampa mzuka Chilunda
Bao lampa mzuka Chilunda
Read also