Na mwandishi wetu
Kikosi cha timu ya Simba SC kimeelekea Zanzibar leo Jumanne tayari kwa ajili ya ushiriki wake wa michuano ya Kombe la Muungano 2024 inayotarajia kuanza kuunguruma kesho visiwani humo.
Wekundu hao wanatarajia kufungua dimba la michuano hiyo iliyorejea kwa mara nyingine msimu huu kesho Jumatano kwa kuumana na KVZ katika Uwanja wa New Aaman Complex, Zanzibar.
Endapo Simba itafanikiwa kushinda mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza, itakutana na mshindi baina ya Azam na KMKM katika nusu fainali ya pili itakayopigwa keshokutwa Alhamisi Uwanja wa Aaman kuanzia saa 2.15 usiku.
Michuano hiyo ambayo ni maalum kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanzania, Aprili 26, fainali yake inatarajiwa kupigwa Aprili 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa Aaman kuanzia saa 2.15 usiku.
Azam tayari ilishatua visiwani humo tangu jana huku ofisa habari wa timu hiyo, Hasheem Ibwe akieleza kuwa wamekwenda Zanzibar kwa ajili ya kupambana kuhakikisha wanaweka rekodi na kukata kiu ya mashabiki wa soka kwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.
Soka Simba yaelekea Zanzibar
Simba yaelekea Zanzibar
Read also