Na mwandish wetu
Bondia Ibrahim Class ameeleza kuwa kwa sasa yuko kwenye maandalizi makubwa ya kuhakikisha anaibuka na ushindi kwenye pambano lake litakalopigwa Agosti 27, mwaka huu dhidi ya Khamis Muathai kutoka vsiwani Zanzibar.
Pambano hilo ambalo ni la kwanza tangu kuruhusiwa kwa ngumi visiwani Zanzibar litapigwa kwenye Ukumbi wa Mao Tse Tung, Zanzibar.
Class alisema kuwa anaamini ataondoka na ushindi katika usiku huo kwa sababu anahisi hakuna bondia mwingine anayejipanga kimazoezi kama yeye nchini Tanzania hivyo ushindi kwake ni kitu cha kusubiri siku ya tukio ifike.
“Yaani hiyo tarehe 27 sitaki lawama kwa kweli, nawaambia Zanzibar nafanya mazoezi ya kila rangi, nafanya mazoezi ya kila aina na nafanya zaidi ya mara 10, sina imani kwa kwei hapa Tanzania kama kuna bondia anafanya mazoezi zaidi yangu na hilo nitawathibitishia tarehe 27, Khamis ajipange,” alisema Class.
Mbali na pambano hilo, mapambano mengine yatawakutanisha Abdllah Pazi ‘Dulla Mbabe’ dhidi ya Banja Hamis na Karim Mandonga atakayezichapa na Muller Junior.
Ngumi Ibra Class aanza mikwara
Ibra Class aanza mikwara
Read also