Paris, Ufaransa
Ushindi wa jumla wa mabao 6-5 ambao Real Madrid imeupata dhidi ya Man City umewashtua na kuwashangaza kama si kuwaduwaza wengi. Mmoja wa watu waliojikuta katika hali hiyo ni nyota wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi.
“Acha utani, haiwezi kabisa kuwa kweli,” huo ni ujumbe mfupi wa Messi kwenye mitandao ya kijamii akimtumia mchezaji mwenzake wa Argentina, Sergio Aguero wakati akizungumzia ushindi wa Real Madrid kwenye mechi hiyo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Real Madrid ikiwa nyumbani jana usiku, iliingia uwanjani ikiwa imefungwa mabao 4-3 katika mechi ya kwanza ugenini lakini ilifanya maajabu na kutoka na ushindi wa mabao 3-1 huku mabao yao yakifungwa na Rodrigo aliyefunga mawili na la mwisho lilifungwa na Benzema kwa mkwaju wa penalti wakati bao pekee la City lilifungwa na Mahrez katika dakika ya 73.
Messi ambaye amejipatia mafanikio akiwa Barcelona, kwa sasa anaichezea PSG, alibaki katika hali ya mshangao kwa namna Real Madrid ilivyopambana na kubadili matokeo ya mchezo na sasa inajiandaa kuumana na Liverpool katika mechi ya fainali itakayopigwa Mei 28, jijini Paris, Ufaransa.
Aguero, ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa City akiweka rekodi ya kuvutia ya mabao, naye hakuamini macho yake pale Real Madrid ilipopata mabao mawili ya Rodrigo kabla Benzema hajamalizia kazi kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa baada ya mchezaji huyo kuchezewa rafu.
Kwa sasa Aguero ni mchambuzi wa soka, kazi ambayo alianza kuifanya baada ya kustaafu soka mapema hivi karibuni wakati akikipiga katika klabu ya Barcelona aliyojiunga nayo akitokea City.
Kimataifa Real Madrid yamduwaza Messi
Real Madrid yamduwaza Messi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
