Na mwandishi wetu
Tamasha ya Yanga Day limeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 2-1 na timu ya Aigles du Congo ya DR Congo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Jumapili Agosti 8, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliotanguliwa na shamrashamra za kuwatambulisha wachezaji wapya wa Yanga kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-26, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na mchezaji wao mpya, Peter Shalulile.
Shalulile alifunga bao hilo katika dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti lakini iliwachukua Aigles dakika 10 kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Talasy Tonny na kuzifanya timu ziende mapumziko zikiwa sare.
Aigles waliandika bao la pili katika dakika ya 65, mfungaji kwa mara nyingine akiwa Tony na kuifanya timu yake itoke uwanjani na ushindi.
Mchezo huo umelipa benchi la ufundi la Yanga nafasi nzuri ya kukifanyia tathmini kikosi hicho kipya kabla ya kuanza mbio za kulitetea taji la Ligi Kuu NBC msimu wa 2026-27.
Yanga itaanza kuufungua msimu mpya kwa kuumana na mahasimu wao Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Jumatano Agosti 12, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Kimataifa Tamasha Yanga Day laingia doa
Tamasha Yanga Day laingia doa
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
