London, England
Mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya England, Harry Kane ameibuka mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or msimu wa 2025-26 na kuibeba England baada ya kuikosa tuzo hiyo kwa miaka 25.
Mara ya mwisho tuzo hiyo kubebwa na mchezaji wa England ilikuwa mwaka 2001 ambapo ilibebwa na Michael Owen, mshambuliaji wa zamani wa England na timu za Liverpool, Real Madrid na Newcastle.
Ushindi wa Kane ulitangazwa katika hafla iliyofanyika jijini London, usiku wa Jumapili Oktoba 25, 2026 na kumfanya mshambuliaji huyo aingie katika orodha ya wachezaji watano wa England waliowahi kubeba tuzo hiyo.
Wachezaji wengine wa England waliowahi kubeba tuzo hiyo mbali na Kane na Owen ni Stanley Matthews mwaka 1956, Bobby Charlton mwaka 1966 na Kevin Keegan aliyebeba mwaka 1978 na 1979.
Kwa upande mwingine Kane pia anakuwa mchezaji wa kwanza wa Bayern Munich kubeba tuzo ya Ballon d’Or tangu Karl-Heinz Rummenigge afanye hivyo mwaka 1981.
Kane, 33, katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo alikuwa akichuana na Kylian Mbappe wa Real Madrid aliyeshika nafasi ya pili na Lamine Yamal wa Barcelona aliyeshika nafasi ya tatu.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Kane alisema kwamba watu wengi hawakutarajia yeye kuibuka mshindi na pengine hata yeye hakutarajia kufikia hatua hiyo kubwa.
“Nimepitia mengi ya kupanda na kushuka, hususan mwanzoni mwa maisha yangu ya soka, sikuwa mtu ambaye watu wangetarajia niwe supa staa,” alisema Kane.
Alisema kwamba alikuwa akifanya mambo yake kwa bidii na ilikuwa kama mtu aliyekuwa akipambana na hisia zake na kupitia katika jambo hilo alilazimika kuonesha namna anavyojiamini na mwenye shauku.
Kane alifunga mabao 61 katika mechi 51 za klabu kwa msimu uliopita akiweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee wa Bayern na kwenye ligi kubwa za Ulaya kuweka rekodi ya kufunga mabao mengi kwa msimu mmoja.
Ukijumlisha na mabao aliyoifungia timu ya taifa ya England kwa msimu huo mmoja, Kane anakuwa amefunga jumla ya mabao 73 katika mechi 65.
Ushindi wa Kane hata hivyo umekuwa ukilalamikiwa kwa kuwa katika msimu uliopita hakuweza kubeba taji kubwa la Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo aliishia hatua ya nusu fainali kama ilivyokuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Kwa upande wake Mwana Mfalme wa Uingereza, Prince William alimpongeza Kane ambaye pia amewahi kutamba na klabu ya Tottenham ya England kwa kutwaa tuzo hiyo akisema ni nahodha bora wa England na mchezaji wa aina yake.
