Na mwandishi wetu
Klabu ya Tabora United imetangaza kunasa saini ya kiungo wa zamani wa Yanga, Papy Tshishimbi kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Tabora iliyokuwa ikifahamika kwa jina la Kitayosce ambayo imepanda kushiriki Ligi Kuu NBC msimu huu imemtangaza leo Jumatano mchezaji huyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii wakimkaribisha katika familia yao ya soka wakiamini ujio wake utawabeba zaidi.
“Karibu kwenye familia kubwa ya Nyuki wa Tabora kiungo wa mpira, Papy Kabamba Tshishimbi. Sasa naye ni nyuki mpya wa Tabora,” ilieleza sehemu ya taarifa ya timu hiyo.
Mchezaji huyo raia wa DR Congo naye alieleza furaha yake ya kujiunga tena na timu hiyo ambayo alijiunga nayo mwaka juzi na kujaribu kuipandisha daraja lakini ilishindikana na sasa amefurahi kuitumikia tena.
“Nilishawahi kuwa hapa msimu fulani, tukacheza hatua ya mtoano kwa bahati mbaya hatukufanikiwa kupita, lakini nafurahi kurudi tena kwenye timu hii lakini safari hii ikiwa ligi kuu tayari,” alisema kwa kifupi kiungo huyo aliyewahi pia kukipiga Ihefu na AS Vita ya DR Congo.
Soka Tshishimbi asaini Tabora United
Tshishimbi asaini Tabora United
Read also