Na mwandishi wetu
Mechi ya mahasimu wa jadi nchini Tanzania, Simba na Yanga, iliyopangwa kuchezwa Jumapili Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, sasa itachezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Ijumaa Aprili 24, 2026 imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa kwa kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao pia upo jijini Dar es Salaam, unafanyiwa matengenezo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka idara ya mawasiliano ya bodi hiyo, mechi hiyo itaanza majira ya saa 12 jioni kwenye uwanja huo unaomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa.
Klabu husika za Simba na Yanga pamoja na wadau wengine wa Ligi Kuu NBC tayari zimepewa taarifa za mabadiliko hayo ya uwanja ili kuhakikisha maandalizi yanaanza mara moja ili kuhakikisha mchezo huo unafanyika katika kiwango cha juu cha ubora na hadhi ya Ligi Kuu NBC.
Uamuzi wa kuhamisha uwanja kwa ajili ya mechi hiyo umeanza kuibua maswali miongoni mwa mashabiki wa soka huku baadhi wakihoji kiini hasa cha mabadiliko hayo.
Mashabiki wengine wanatilia shaka uwezo wa uwanja kwa mechi kubwa kama ya Simba na Yanga ingawa katika maeneo mengine yakiwamo ya kuchezea uwanja huo unaochukua mashabiki wasiozidi 15,000 upo katika ubora.
Kimataifa Simba, Yanga kukipiga jeshini
Simba, Yanga kukipiga jeshini
Related posts
Read also
