Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Miguel Gamondi anatarajia kushiriki katika warsha maalum na makocha wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Zanzibar.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana Ijumaa Aprili 17, 2026 ilieleza kuwa warsha hiyo itafanyika Aprili 20, 2026 kwenye Ukumbi wa Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Katika taarifa hiyo hata hivyo haikuwekwa wazi nini hasa mada itakayojadiliwa na Gamondi na makocha hao wa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo ambayo kwa sasa ipo katika raundi ya 23.
Timu zinazoshiriki Ligi Kuu Zanzibar ni pamoja na JKU, Chipukizi, Junguni, Kipanga, KMKM, Fufuni, Uhamiaji, Polisi, Zimamoto, Mafunzo, KVZ, Mwembemakumbi City, NS Town, New King, Mlandege na Malindi.
Tangu achaguliwe kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars mwishoni mwa mwaka jana, hii itakuwa mara ya kwanza kwa Gamondi kupata nafasi ya kukaa pamoja na makocha wa timu za Ligi Kuu Zanzibar.
Kimataifa Gamondi, makocha Zanzibar kuteta
Gamondi, makocha Zanzibar kuteta
Read also
