Seoul, Korea Kusini
Korea Kusini imetangaza kikosi cha wachezaji wake kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia akiwamo mshambuliaji majeruhi wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min.
Son mwenye umri wa miaka 30 amekuwa katika hatihati ya kuwamo kwenye kikosi hicho baada ya kufanyiwa operesheni ya jicho aliloumia mapema mwezi huu wakati akiiwakilisha Tottenham kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Marseille lakini Jumatano iliyopita aliwahakikishia mashabiki wa Korea Kusini kwamba atakuwa fiti kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia.
Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar, zitaanza rasmi kutimua vumbi Novemba 20 mwaka huu ambapo Korea Kusini inayonolewa na kocha Paulo Bento itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 24 dhidi ya Uruguay.
Jumatano iliyopita kocha Bento ambaye anatokea nchini Ureno, aliwahi kuelezea wasiwasi wake kuhusu Son aliposema, “hatuna taarifa hizo (za Son kuwa fiti) tunawasiliana naye, pamoja na timu ya madaktari wa Tottenham, tunahitaji kusubiri na kuangalia hali yake siku baada ya siku lakini bado muda tunao.”
Son baada ya kuitwa inadaiwa huenda akalazimika kuvaa kifaa maalum cha kuzuia jicho kama atacheza mechi katika fainali hizo ambapo mbali na Uruguay, Korea Kusini pia itaumana na Ghana na Ureno ambazo zote zipo Kundi H.
Kikosi kamili cha Korea Kusini ni kama ifuatavyo…
Makipa: Kim Seung-gyu (Al Shabab), Jo Hyeon-woo (Ulsan Hyundai), Song Bum-keun (Jeonbuk Motors)
Mabeki: Kim Min-jae (Napoli), Kim Jin-su (Jeonbuk Motors), Hong Chul (Daegu FC), Kim Moon-hwan (Jeonbuk Motors), Yoon Jong-gyu (FC Seoul), Kim Young-gwon (Ulsan Hyundai), Kim Tae-hwan (Ulsan Hyundai), Kwon Kyung-won (Gamba Osaka), Cho Yu-min (Daejon Citizen)
Viungo: Jung Woo-young (Al Sadd), Na Sang-ho (FC Seoul), Paik Seung-ho (Jeonbuk Motors), Son Jun-ho (Shandong Taishan), Song Min-kyu (Jeonbuk Motors), Kwon Chang-hoon (Gimcheon Sangmu), Lee Jae-sung (Mainz), Hwang Hee-chan (Wolverhampton Wanderers), Hwang In-beom (Olympiacos), Jeong Woo-yeong (Freiburg), Lee Kang-in (Real Mallorca)
Washambuliaji: Hwang Ui-jo (Olympiacos), Cho Gue-sung (Jeonbuk Motors), Son Heung-min (Tottenham)
Kimataifa Majeruhi Son aitwa Korea Kusini
Majeruhi Son aitwa Korea Kusini
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
