London, England
Mechi za Ligi Kuu England (EPL) zinatarajia kusimama wikiendi hii ili kutoa nafasi kwa wananchi kuomboleza msiba wa Malkia Elizabeth 11 wa Uingereza aliyefariki jana Alhamisi akiwa na miaka 96.
Sambamba na ligi hiyo ya soka, ligi nyingine za soka za nchi za Wales, Scotland, Northen Ireland pamoja na matukio mengine ya kimichezo ya rugby, kriketi, mbio za farasi na mengineyo yote yanatarajia kusimama kwa ajili ya msiba wa kiongozi huyo wa kifalme ambaye ameongoza katika nafasi hiyo kwa takriban miaka 70.
Kwa hali hiyo mechi za EPL zilizopangwa kuchezwa Jumamosi na Jumapili ni wazi hazitakuwapo na haijaweza kueleweka mara moja hali itakuwaje katika mechi za wikiendi inayofuata hasa kwa kuwa Malkia Elizabeth huenda akazikwa Jumapili ijayo.
Inadaiwa mamlaka za Uingereza bado hazijatoa muongozo wowote kuhusu matukio ya kimichezo lakini kilicho wazi ni kwamba baadhi ya mechi za ndani zitasimama kupisha msiba huo kwa utaratibu ambao utapangwa na mamlaka za mchezo husika.
Hata hivyo huenda mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya ambazo kwa kawaida huchezwa Jumanne na Jumatano zikaendelea kama kawaida kwa kuwa mechi hizo ratiba zake hupangwa na Uefa na mamlaka za soka Uingereza hazina uamuzi katika upangaji wa ratiba za mechi hizo.
Mfano ni mechi ya Chelsea na Red Bull Salzburg ambayo itapigwa Jumatano kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
Kimataifa Msiba wa Malkia waahirisha mechi EPL
Msiba wa Malkia waahirisha mechi EPL
Related posts
Read also
