Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa timu ya JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema usajili wa nyota wa zamani wa Simba, Shiza Kichuya utairudisha timu yake nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Akizungumza na GreenSports leo Jumanne, kocha huyo alisema uzoefu wake kwenye ligi pamoja na kucheza timu kubwa za Mtibwa Sugar, Simba na Namungo FC kutaongeza kitu kwao.
“Kichuya ni mchezaji mzoefu, lakini ameshapata mafanikio akiwa na Simba pia aliwahi kucheza soka la kulipwa nje, hivyo vyote vitatuongezea kitu sisi lakini pia wachezaji vijana watapata muda wa kujifunza kutoka kwake,” alisema Malale.
Pia Malale alisema mechi zilizopita walikuwa na mapungufu makubwa ya winga hivyo ujio wa mkongwe huyo umewasaidia kuwa na nafasi pana ya kubadili mifumo ya kucheza kulingana na mpinzani.
JKT Tanzania ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC, ikikusanya pointi 16 katika michezo 14 iliyocheza hadi sasa.
Soka Kichuya kuipaisha JKT Tanzania
Kichuya kuipaisha JKT Tanzania
Read also
