London, England
Klabu ya Tottenham Hotspur inajipanga kuingia katika vita ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Crystal Palace, Eberechi Eze (pichani) ambaye pia anawaniwa na Arsenal.
Eze, 27, kwa sasa ana miaka miwili katika mkataba wake na Palace ingawa katika mkataba huo kuna kipengele kinachompa nafasi ya kuihama timu hiyo kwa dau linalodaiwa kufikia Pauni 68 milioni.
Kabla ya kuanza mchakato wa kuinasa saini hiyo, wanachofanya Spurs kwa wakati huu ni kujiridhisha iwapo kipengele hicho kimeshapitwa na wakati au bado kinaendelea.
Kwa upande wa Arsenal, kwa muda mrefu imekuwa ikivutiwa kumsajili Eze lakini suala la kulipa Pauni 68 milioni limeonekana kuitatiza klabu hiyo na habari za ndani zinadai kuwa ili kufanya usajili huo ni lazima wauze wachezaji.
Baadhi ya wachezaji wa Arsenal ambao inadaiwa wanaweza kutupwa sokoni na hivyo kuwa rahisi kuinasa saini ya Eze ni pamoja na Reis Nelson, Oleksandr Zinchenko, Fabio Vieira na Leandro Trossard.
Palace nayo haifurahii kumuacha Eze aondoke lakini inatambua kuwa mkataba wa mchezaji huyo unafikia mwisho mwaka 2027 na haoneshi dalili zozote za kuongeza mkataba kumfanya aendelee na timu hiyo baada ya mwaka 2027.
Eze ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya England, alitoa mchango mkubwa kwa Palace hadi kubeba Kombe la FA mwishoni mwa msimu uliopita wa 2024-25.
Tangu ajiunge na Palace mwaka 2020 akitokea Queen’s Park Rangers, Eze ana rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao 34 na kutoa asisti 23 katika mechi 146 za Ligi Kuu England.
Kimataifa Arsenal, Spurs vitani kumsaka Eze
Arsenal, Spurs vitani kumsaka Eze
Related posts
Read also
