London, England
Kiungo wa West Ham na timu ya Taifa ya England, Declan Rice (pichani) ambaye anawaniwa na timu za Arsenal na Manchester City inadaiwa anapendelea zaidi kujiunga Arsenal badala ya Man City.
Uamuzi huo wa Rice umekuja baada ya Man City kudaiwa kuingia katika mbio za kumtaka mchezaji huyo wakati huu ofa mbili za Arsenal zikiwa zimekataliwa ikiwamo ya mwisho ya Pauni 90 milioni.
Kitendo cha Man City kumtaka mchezaji huyo kinaiweka pagumu Arsenal na haijaweza kufahamika mara moja kama timu hiyo itakuwa tayari kushindana katika kuisaka saini ya mchezaji huyo.
Man City tayari imeonesha nia ya kumsajili Rice ikidaiwa kuwa tayari kutoa Pauni 100 milioni ikiamini mchezaji huyo ni mtu sahihi kuziba pengo la kiungo wao, Ilkay Gundogan aliyehamia Barcelona.
Kwa upande mwingine uamuzi wa Rice kuichagua Arsenal linakuwa jambo zuri kwa kocha Mikel Arteta ambaye anaamini mchezaji huyo ni nahodha wa baadaye wa timu yake na sasa wanajiandaa kupeleka West Ham ofa yao kwa mara ya tatu.
Rice amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha West Ham akiisaidia timu hiyo kubeba taji la Europa Conference Ligi lakini pia ameonesha uwezo katika kikosi cha timu ya Taifa ya England na hadi sasa hatma yake imekuwa mjadala kila kona hasa baada ya yeye mwenyewe kusema kwamba angependa kusaka changamoto katika klabu nyingine.
Kimataifa Rice aikataa Man City, aitaka Arsenal
Rice aikataa Man City, aitaka Arsenal
Read also