Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Francis Baraza amesema mchezo wao ujao dhidi ya Yanga hautakuwa rahisi ingawa wamejipanga kuondoka na pointi zote tatu.
Kocha huyo amesema leo Jumamosi timu wanayoenda kucheza nayo ni mabingwa watetezi katika nchi hivyo wanakwenda kwa tahadhari kubwa.
“Tutacheza kwa kuwaheshimu huku tukitumia mashambulizi ya kushtukiza kwenye lango lao, lengo letu ni pointi tatu na kama tutajipanga vizuri uwezekano wa kuzipata upo,” alisema Baraza.
Mbali na Baraza, naye kiungo Mtenje Albano alisema maandalizi yao kama wachezaji ni mazuri wanaamini mchezo utakuwa mzuri lakini mgumu kwa sababu Yanga wanaifahamu ni timu kubwa lakini Dodoma Jiji ni bora pia.
Mchezo huo utachezwa keshokutwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na Yanga kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Soka Baraza aanza hesabu za kuivaa Yanga
Baraza aanza hesabu za kuivaa Yanga
Read also
