Barcelona, Hispania
Habari kwamba klabu ya Barcelona ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford imeibuka tena huku ikidaiwa kwamba mazungumzo yameanza.
Inadaiwa kwamba Barcelona au Barca imeamua kumrudia mchezaji huyo kwa nguvu mpya baada ya mipango yao ya kutaka kumsajili Luis Diaz kutoonesha dalili za mafanikio.
Diaz, nyota wa Liverpool naye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Barcelona hapo hapo mipango ya Barca kumsajili Nico Williams ikikwama mapema baada ya mchezaji huyo kuamua kubaki Bilbao.
Uwezekano wa Barcelona kumpata Rashford ni mkubwa hasa kwa kuwa mchezaji huyo amewahi kusema kwamba anataka kuihama timu hiyo na kutafuta changamoto nyingine.
Rashford, 27, ana mkataba na Man United ambao unafikia mwisho mwaka 2028 wakati sehemu ya msimu uliopita wa 2024-25 alilazimika kucheza kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa.
Uamuzi wa kujiunga na Villa ulikuja baada ya kutokea sintofahamu kati yake na kocha Ruben Amorim hali iliyosababisha Rashford kutokuwa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza cha Man United.
Amorim aliwahi kusema kwamba mshambuliaji huyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya England hajitumi kama inavyotakiwa lakini pia akampa uhuru wa kuamua kubaki au kuondoka kama ataona inafaa kufanya hivyo.
Wakati huo huo winga wa Man United, Jadon Sancho naye anatajwa kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Juventus ya Italia.
Sancho naye mambo yake hayakuwa mazuri Man United na msimu uliopita aliichezea Chelsea kwa mkopo na kufanikiwa kufunga mabao matatu katika mechi 31 alizocheza.
Kimataifa Barca yarudi kwa Rashford
Barca yarudi kwa Rashford
Read also
