Na mwandishi wetu
Bondia wa ngumi za kulipwa, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ amesema yuko tayari kwa pambano lake la kimataifa lisilo la ubingwa dhidi ya Callum Simpson wa Uingereza litakalopigwa Machi 31, mwaka huu.
Pambano hilo la raundi 10 litafanyika kwenye ukumbi wa O2 Arena, Greenwich jijini London ambapo Dullah anaenda kwenye pambano hilo akiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda pambano lake la mwisho la kimataifa la Januari Mosi.
Katika pambano hilo lililofanyika jijini Tanga, Dulla alimbwaga Limbani Lano wa Malawi kwa matokeo ya pointi za majaji wote watatu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dulla alisema kama bondia muda wote anapaswa kuwa fiti ili aweze kucheza mapambano mengi na kutwaa mikanda ili apande kwenye viwango vya ubora.
“Kazi yangu ni ngumi na kuwafanya wapenzi wa ngumi wafurahi ndio maana najifua ili nishinde kila pambano lililo mbele yangu japokuwa siwezi kumzungumzia mpinzani nitakayekutana naye,” alisema Dullah.
Ngumi Dulla Mbabe apeleka ubabe Uingereza
Dulla Mbabe apeleka ubabe Uingereza
Read also