Na mwandishi wetu
Simba na Yanga zitakaa siku tatu hadi nne baada ya michezo yao ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly na Mamelodi Sundowns kisha kucheza michezo ya Kombe la FA (ASFC).
Timu zote mbili zimeshacheza mechi za kwanza kwenye Uwanja wa Mkapa ambapo Simba ilifungwa na Ahly ya nchini Misri bao 1-0 wakati Yanga ikitoka sare ya 0-0 na Mamelodi ya Afrika Kusini.
Mechi za marudiano na timu hizo zitachezwa Aprili 5 ambapo timu hizo zitakuwa ugenini, Simba ikiwa nchini Misri katika jiji la Cairo wakati Yanga itakuwa Afrika Kusini mjini Pretoria.
Baada ya mapumziko ya siku tatu hadi nne, timu hizo zitaanza kujipanga na FA, Simba itacheza na Mashujaa Aprili 9, ugenini kwenye Uwanja wa Tanganyika, Kigoma na Yanga ikitarajiwa kuelekea Dodoma, Uwanja wa Jamhuri kuwakabili Dodoma Jiji April 10, mwaka huu.
Ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inaonesha kuwa michuano hiyo ya raundi ya nne kuisaka robo fainali, itaanza Aprili 2 na kutakuwa na mechi moja kila siku ambapo Namungo itaikabili Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.
Mechi nyingine ni Singida dhidi ya Tabora United, Coastal dhidi ya JKT Tanzania, KMC itaivaa Ihefu na Azam FC wataumana na Mtibwa Sugar.
Soka Simba, Yanga kibaruani FA
Simba, Yanga kibaruani FA
Read also