London, England
Kocha mpya wa Chelsea, Graham Potter amewaaga mashabiki wa Brighton kwa barua akiwaambia kwamba amelazimika kuikimbilia fursa mpya katika klabu ya Chelsea.
Potter ameyasema hayo katika barua ya wazi kwenda kwa mashabiki akiwaelezea sababu iliyomfanya kuachana na Brighton aliyodumu nayo kwa miaka mitatu na kujiunga na Chelsea Alhamisi iliyopita.
“Kwa baadhi yenu najua kwamba mabadiliko yamekuja ghafla sana na katika soka inaweza kuwa vigumu kukubali, pengine nisingeweza kuwashawishi nyinyi wote mnisamehe kwa kuondoka kwangu lakini walau napenda kuchukua nafasi hii kuwaambia ahsanteni.”
Potter mwenye umri wa miaka 47 ambaye anajiunga na Chelsea kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel aliyetimuliwa aliongeza, “Natumaini mtaelewa kwamba katika kipindi hiki cha maisha yangu ya ukocha nimeona nalazimika kuikamata fursa mpya.”
Potter, kocha wa zamani wa timu za Ostersunds FK na Swansea City ameiongoza Brighton hadi kushika nafasi ya tisa katika Ligi Kuu England msimu uliopita, hayo yakiwa ni mafanikio makubwa katika historia ya timu hiyo.
Katika msimu huu hadi sasa timu hiyo anaiacha ikiwa katika nafasi ya nne baada ya kushinda mechi nne, sare moja katika mechi zao sita za Ligi Kuu England.
Potter ambaye mechi yake ya mwisho iliyopigwa Septemba 4, Brighton iliichapa Leicester City mabao 5-2 aliongeza, “Wakati huo sikufahamu kama ingekuwa ndio mwisho lakini nikirudi nyuma naona tulivyocheza vizuri, kuna mambo mengi mazuri katika klabu.”
Kimataifa Potter awaaga mashabiki Brighton kwa barua
Potter awaaga mashabiki Brighton kwa barua
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
