Riyadh, Saudi Arabia
Klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia imepania kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na tayari imemtengea Pauni 118 milioni licha ya klabu yake kusisitiza kwamba mchezaji huyo hauzwi.
Salah kwa sasa ni mmoja wa washambuliaji muhimu na tegemeo katika kikosi cha Liverpool na kocha Jurgen Klopp amekuwa mstari wa mbele kusisitiza kwamba hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo kutoka Misri.
Wakati msimamo wa Liverpool ukiwa hivyo, vyombo kadhaa vya habari vya Uingereza vimeripoti hii leo kuwa Al-Ittihad inafanya kila liwezekanalo kumshawishi mshambuliaji huyo aachane na Liverpool jambo ambalo likifanikiwa litamkera mno Klopp.
Salah, 31, hajaweka wazi msimamo wake wa mwisho lakini ushawishi wa Al-Ittihad unaweza kumfanya achukue maamuzi magumu ya kuachana na Ligi Kuu England (EPL) na kuhamia Saudi Pro Ligi iliyojaa mastaa mbalimbali wa soka duniani akiwamo Sadio Mane aliyewahi kucheza naye Liverpool.
Kesho Ijumaa usiku ambayo ni siku ya mwisho ya usajili wa majira ya kiangazi, ni siku inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki duniani kote kwani lolote linaweza kutokea kuhusu wachezaji mbalimbali akiwamo Salah kama ni kubaki au kuondoka Liverpool.
Kimataifa Al-Ittihad yamkomalia Salah
Al-Ittihad yamkomalia Salah
Read also