Na mwandishi wetu
Siku moja baada ya kocha Hans Pluijm atangazwe kuachwa na klabu ya Singida Fountain Gate, amesema anaamini timu hiyo ipo kwenye mstari mzuri wa mafanikio na itafika mbali kimataifa.
Uongozi wa Singida ulitangaza kuachana na kocha huyo raia wa Uholanzi jana ikiwa siku ni tatu zimepita tangu aivushe raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuifunga JKU jumla ya mabao 4-3.
Pluijm ameiambia GreenSports kuwa asingependa kuzungumzia kuhusu kuachana na timu hiyo kwa sasa bali anachojua ni miongoni mwa timu zenye mipango mizuri na anaitakia kila la heri.
“Sitaki kuzungumzia kwa undani kuhusu kuondoka Singida lakini ni kati ya timu ninazozitumainia sana kufika mbali kwenye ligi kuu na hata michuano ya kimataifa kutokana na mipango waliyonayo,” alisema Pluijm.
Alisema anawapenda mashabiki wa Singida na Watanzania kwa ujumla kutokana na sapoti wanayompa na mapenzi ya dhati waliyonayo katika soka, ndio maana huvutiwa kurejea kufundisha Tanzania.
Kabla ya Singida aliyoipeleka kwenye michuano ya klabu Afrika msimu huu kwa mara ya kwanza, Pluijm pia amewahi kuzinoa Yanga na Azam kwa nyakati tofauti.
Soka Pluijm: Singida FG itafika mbali
Pluijm: Singida FG itafika mbali
Read also