London, England
Straika wa Fulham, Aleksandar Mitrovic amefungiwa mechi nane kwa kosa la kumsukuma mwamuzi Chris Kavanagh katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Man United.
Tume huru imemkuta mchezaji huyo kutoka Serbia na hatia hivyo atakosa mechi tatu baada ya kupewa kadi nyekundu, mechi tatu nyingine kwa kufanya fujo na mbili kwa kutoa vitisho na lugha chafu.
Mchezaji huyo pia atatakiwa kulipa faini ya Pauni 75,000 wakati kocha wake, Marco Silva yeye ameadhibiwa kukosa mechi mbali baada ya kupewa kadi nyekundu.
Katika makosa hayo Silva pia anadaiwa kurusha chupa ya maji eneo alilokuwa mwamuzi msaidizi pamoja na kauli alizozitoa wakati akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya timu yake kufungwa.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 alikiri kufanya mambo yasiyo ya kiuanamichezo kwa waamuzi pamoja na kauli zisizopendeza alizozitoa baada ya mechi lakini alikana kurusha chupa ya maji.
Silva aliwahi kutoa taarifa wiki iliyopita akimuomba msamaha mwamuzi Kavanagh na kujutia alichokifanya katika tukio la mechi hiyo iliyochezwa Machi 19 mwaka huu na Fulham kulala kwa mabao 3-1 licha ya kuwa ya kwanza kupata bao.
Kwa upande wa Mitrovic adhabu hiyo itamfanya msimu huu aiwakilishe Fulham katika mechi tatu tu za mwisho, ya kwanza ikiwa mechi dhidi ya Southampton itakayochezwa Mei 13 mwaka huu.
Kimataifa Straika Fulham afungiwa mechi 8
Straika Fulham afungiwa mechi 8
Related posts
Read also