Paris, Ufaransa
Washambuliaji wa timu ya Paris St-Germain (PSG) ya Ufaransa, Lionel Messi na Neymar wako mbioni kuihama timu hiyo, Neymar akiwaniwa na Chelsea na Messi akijipanga kurudi Barca.
Neymar ambaye kwa sasa ni mgonjwa, kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, PSG inajipanga kumuuza mchezaji huyo huku Chelsea ikitajwa kuonyesha dalili za kutaka kumnunua.
Awali iliwahi kuelezwa kwamba mabosi PSG ndio walioshikilia mpango wa kuuzwa kwa Neymar tangu msimu uliopita lakini wazo hilo lilibadilika baada ya mchezaji huyo kuonekana kuwa kivutio tangu kuanza kwa msimu huu.
Hata hivyo Machi mwaka huu Neymar aliumia na kuelezwa kwamba atakosa mechi zote za msimu uliobaki jambo ambalo inadaiwa kuchangia kuibuka upya kwa mpango wa kumuuza mchezaji huyo.
Kuhusu suala la Messi, klabu yake ya zamani ya Barca kwa kipindi kirefu imekuwa ikitaka kumrudisha mchezaji huyo ambaye inadaiwa ana nia ya kufanya hivyo na ndio maana hajaongeza mkataba PSG na haonyeshi dalili za kufanya hivyo.
Barca hata hivyo watakuwa na kazi kubwa kumpata Messi kwani inadaiwa kwamba thamani ya kumpata inaweza kufikia Pauni 88 milioni.
Kwa upande mwingine tayari zipo habari kwamba Messi pia ametangaziwa dau nono nchini Saudi Arabia katika klabu ya Al Hilal ya huko.
Iwapo mpango wa Messi kwenda Saudi Arabia utafanikiwa atakuwa ameungana na mchezaji mwenzake nyota wa zamani wa Real Madrid na Man United, Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Al Nassr ambao ni mahasimu wa Al Hilal.
Kimataifa Messi, Neymar kuondoka PSG
Messi, Neymar kuondoka PSG
Read also
