New York, Marekani
Mwanamitindo na staa wa vipindi vya televisheni,, Paris Hilton kwa sasa ni mama baada ya kujifungua mtoto wa kiume ambaye anakuwa mtoto wake wa kwanza ingawa kwa mumewe, Carter Reum anakuwa mtoto wa pili.
Taarifa ya Paris kupata mtoto ilipatikana kwenye mtandao wa Instagram ambapo alionyesha picha akiwa amemshika mkono mtoto huyo na kusema, “Tayari unapendwa kuliko inavyoweza kuzungumzwa.”
Bado haijajulikana ni lini mtoto huyo alizaliwa licha ya habari za awali kudai kwamba alizaliwa Jumanne na pia jina la mtoto huyo bado halijajulikana ingawa inafahamika kuwa alipata mtoto huyo kupitia kwa mwanamke mwingine (Surrogate).
Baada ya kufunga ndoa mwaka 2021, Paris Hilton na mumewe Carter waliwahi kuzungumzia nia yao ya kuwa wazazi kwa kupitia mwanamke mwingine kama ambavyo amefanya staa wa vipindi vya televisheni, Khloe Kardashian ambaye alipata mtoto wa kiume kwa utaratibu huo huo.
Paris ndio aliyekuwa akilizungumza sana jambo hilo ambapo mara ya mwisho alisema, angependa afurahie mwaka wake wa kwanza wa ndoa lakini wakati huo huo alikuwa akijiandaa kuwa mama.
“Wakati wote imekuwa ndoto yangu muwa mama na nina furaha mimi na Carter tumekutana, tuna furaha kuianza familia pamoja na mioyo yote imegubikwa upendo kwa mtoto wetu wa kiume,” alisema Paris Hilton.
Kwa miaka kadhaa, Paris Hilton alikuwa akijaribu kufuta uvumi kwamba alikuwa na tatizo la kupata mtoto, alikuwa akiupinga uvumi huo na wakati mwingine kusisitiza kuwa yeye na mumewe wanaweka mambo sawa kwa ajili ya kupata mtoto.
Hollywood Paris Hilton apata mtoto
Paris Hilton apata mtoto
Related posts
Read also