Na mwandishi wetu
Hatimaye Yanga SC imeweka wazi kumsajili aliyekuwa beki wa kati wa timu ya SC Villa ya Uganda, Gift Fred.
Tangu majuzi kulivuma taarifa za kusajiliwa kwa beki huyo kwa mkataba wa miaka mitatu, taarifa ambazo GreenSports ilithibitishiwa na ofisa mmoja wa Yanga huku ikiripotiwa wamefanikiwa kumnasa baada ya kumaliza kandarasi yake Villa.
Beki huyo aliyekuwa akiiongoza Villa ametambulishwa rasmi na Yanga jioni ya Jumanne hii kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
“Gift Fred, tazama huyu mwamba, washambuliaji wenu watatoa sana shikamoo msimu huu,” yalieleza maelezo ya chapisho la Yanga yaliyoambatana na picha ya mchezaji huyo akiwa amevaa jezi za msimu ujao wa timu hiyo.
Mchezaji huyo ambaye ameanza kuitwa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ Januari, mwaka huu akiwa ameshacheza mechi tano mpaka sasa, anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa Yanga kuelekea msimu ujao.
Mchezaji mwingine ambaye tayari ametambulishwa na Yanga ni beki wa kushoto, Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate zamani Singida Big Stars.
Soka Beki Gift Fred rasmi Yanga
Beki Gift Fred rasmi Yanga
Read also