Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys na kuipa zawadi ya Sh milioni 500.
Pongezi hizo zimekuja baada ya timu hiyo kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17 ikiitoa Misri kwa penalti 4-3 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa mjini Rabat, Morocco
Sambamba na pongezi na fedha hizo, Rais Samia pia ameahidi kuwapa viwanja wachezaji hao mkoani Morogoro kama wakifanikiwa kuibwaga Senegal na kubeba taji la michuano hiyo.
Ahadi hiyo ya Rais Samia iliwekwa wazi na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ambaye akiwa ofisini kwake mjini Dodoma ambapo alisema kiongozi huyo mkuu wa nchi amewapongeza wachezaji hao kwa jinsi walivyoiwakilisha vyema nchi kimataifa.
“Rais ameelekeza kwamba katika kuthamini mafanikio yao kwa kufikia hatua ya fainali anawapa zawadi y Sh milioni 500,” alisema Dk Nchemba.
Dk Nchemba alifafanua kuwa timu hiyo ikibeba taji kila mchezaji atapewa kiwanja mjini Morogoro na kuongeza kuwa Serikali imeandaa ndege maalum kwa ajili ya wachezaji hao watakaporejea nchini baada ya mechi hiyo.
Wakati huo huo, kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa maendeleo ya soka wa Fifa, ameipongeza timu hiyo kwa mafanikio iliyoyapata dhidi ya timu imara iliyokutana.
Wenger alisema kwamba anaamini kuwa timu hiyo itaonekana kwenye fainali za Kombe la Dunia hivi karibuni.
Serengeti sasa inasubiri kuumana na timu ya taifa ya Senegal katika mechi ya fainali ambayo itachezwa usiku wa Jumanne, Juni 2, 2026.
Kimataifa Rais Samia aipongeza Serengeti Boys, awajaza noti
Rais Samia aipongeza Serengeti Boys, awajaza noti
Read also
