Na mwandishi wetu
Timu ya Pamba FC, ambayo iko chini ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza imemtangaza Mbwana Makata (pichani kulia) kuwa kocha wao mkuu mpya kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Picha zilizowekwa mtandaoni na timu hiyo leo Jumanne zimemuonesha Makata akisaini mkataba huo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla ambaye amedhamiria kuipandisha Pamba Ligi Kuu NBC msimu ujao.
Mbali ya kumtangaza Makata, timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Championship pia imeeleza kuwa Reantus Shija atakuwa msaidizi wa Makata.
Makata ametua Pamba akitokea Ruvu Shooting ambayo imeshuka daraja baada ya kufanya vibaya msimu uliomalizika hivi karibuni na kuungana na Mbeya City na Polisi Tanzania kushiriki Championship msimu ujao 2023-24.
Soka Mbwana Makata kocha mpya Pamba
Mbwana Makata kocha mpya Pamba
Related posts
Read also