Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Mwita wameunda Kamati ya Taifa ya Maandalizi ya michuano ya CHAN 2024 na AFCON 2027 chini ya uenyekiti wa Leodegar Tenga.
Kamati hiyo imetangazwa baada ya kikao cha jana Jumatatu mjini Dodoma kilichohusisha wizara hizo mbili, kikiwa ni maalum kwa ajili ya kujadili maandalizi ya michuano hiyo ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa Afcon ikishirikiana na nchi za Kenya na Uganda.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ni Ayoub Mahmoud, katibu ni Neema Msitha, katibu msaidizi ni Said Marine wakati wajumbe ni Wallace Karia, Suleiman Jabir, Nehemia Mchechu, Wilfred Kidao, Ally Mayay, Ameir Makame, Naima Shaame, Mohamed Abdulaziz na Madundo Mtambo.
Wengine ni Aboubakar Bakhresa, Jacqline Kawishe, Gilead Teri, Ramadhan Dau, Hassan Mabena, Abdul Nsekela, Jumanne Muliro, Abdul Mhinte, Saleh Ally, Hamad Abdallah, Johnson Pallangyo na Kheri Ally.
Mbali na uteuzi huo, pia kikao hicho kilijadili ukarabati wa miundombinu ambayo itatumika katika michuano hiyo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na wakaguzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Soka Mawaziri waunda kamati Afcon, Chan
Mawaziri waunda kamati Afcon, Chan
Read also