Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama leo Jumatano ametangazwa kuibuka kidedea na kuwa Mchezaji Bora wa Simba mwezi Desemba akiwashinda nahodha John Bocco na Shomari Kapombe.
Chama ameshinda tuzo hiyo inayodhaminiwa na Emirate Aluminium Profile baada ya kupigiwa kura na mashabiki wa timu hiyo akizoa jumla ya kura 1,829 huku Bocco akipata kura 1,415 na Kapombe kura 111.
Katika mwezi Desemba, mwaka jana, Chama aliichezea Simba mechi tano ambazo waliibuka na ushindi mechi nne dhidi ya Coastal Union, Geita Gold, KMC, Tanzania Prisons na kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar. Katika mechi hizo, Chama alifanikiwa kufunga mabao mawili na kutoa pasi zilizozaa mabao mara nne.
Chama ambaye anatwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili msimu huu baada ya awali kufanya hivyo mwezi Agosti mwaka jana, anatarajiwa kukabidhiwa kitita cha Sh milioni mbili kwa kunyakua tuzo hiyo.
Wengine waliofanikiwa kutwaa tuzo hiyo msimu huu ni Sadio Kanoute aliyechukua ya mwezi Novemba wakati ya mwezi Oktoba ikitua kwa Mzamiru Yassin na ya Septemba ilikwenda kwa Moses Phiri.
Soka Chama mchezaji bora Simba
Chama mchezaji bora Simba
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
