Na mwandishi wetu
Uongozi wa Mtibwa Sugar umeeleza kumrejesha kocha wake wa zamani wa makipa, Patrick Mwangata na kumsajili mshambuliaji Vitalis Mayanga kutoka Polisi Tanzania.
Mwangata ametua Mtibwa kwa mara nyingine akitokea Ihefu kuja kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mkenya, Razack Siwa (pichai) aliyeachana na timu hiyo hivi karibuni.
Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru amesema wanauamini uwezo wa Mwangata ndiyo maana wamemrejesha kwa mara ya pili ili kusaidiana na benchi la ufundi kuirejesha kwenye makali yake timu hiyo.
Pia usajili wa Mayanga uliotajwa kuwa ni mkataba wa mwaka mmoja alisema hiyo ni kutokana na kuhitaji ufanisi zaidi kwenye eneo la ushambuliaji na Mayanga ameonekana ni mtu sahihi kwa sasa kwa timu hiyo.
“Kifupi bado tunaboresha timu, ndani ya siku mbili hizi zilizobaki pia tunapigania baadhi ya saini kadhaa na kuweka mambo mengine sawa maana tunahitaji kukaa vizuri na kumaliza vizuri kwenye ngwe hii ya lala salama ya Ligi Kuu,” alisema Kifaru.
Soka Mwangata amrithi Siwa Mtibwa Sugar
Mwangata amrithi Siwa Mtibwa Sugar
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
