Milan, Italia
Kocha wa England, Gareth Southgate amesema kwamba ana nia ya kumpigania beki Harry Maguire lakini nafasi yake England itakuwa kwenye utata kama ataendelea kusugua benchi Man United.
Maguire ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa timu ya England hasa katika mbio za Euro 2020, hakuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Man United katika mechi nne zilizopita za Ligi Kuu England ambapo timu hiyo imeshinda mechi nne mfululizo tangu aanze kusugua benchi baada tu ya kuchapwa mabao 4-0 mbele ya Brentford.
“Kimsingi hii si hali nzuri kwa Maguire, tuna wiki chache kabla ya kuanza maandalizi, kwa hiyo angalau unakuwa na dakika 90 mara kadhaa hiyo ni sawa,” alisema Southgate katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi ya England ya Uefa Nations Ligi dhidi ya Italia.
“Wiki nyingine zijazo saba au nane hizo huwa na mambo mengi, lakini huyu ni mchezaji muhimu kwetu, na pia ni muhimu kuwaunga mkono wachezaji wetu bora, hadhi na sifa yoyote niliyonayo naiweka hapo,” alisema.
Katika Uefa Nations Ligi, England ipo katika wakati mgumu kwenye kundi lake baada ya kuvuna pointi mbili tu katika mechi nne ikiwamo vipigo viwili vilivyoshtua wengi dhidi ya Hungary.
Ijumaa hii wataumana na Italia mjini Milan na baada ya hapo watakuwa na mtihani mwingine mgumu, Jumatatu dhidi ya Ujerumani kwenye dimba la Wembley, mechi ambazo pamoja na mambo mengine zina umuhimu kwa timu hiyo katika kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar, Novemba mwaka huu.
Mechi za Uefa Nations Ligi leo
Italia v England
Georgia v North Macedonia
Estonia v Malta
Bulgaria v Gibraltar
Ujerumani v Hungary
Bos-Herze v Montenegro
Finland v Romania
Kimataifa Maguire amuweka pagumu Southgate
Maguire amuweka pagumu Southgate
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
