Manchester, England
Kiungo wa Man United anayetajwa kuwa mbioni kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu, Casemiro inadaiwa amepanga kujiunga na klabu ya Inter Miami ya Marekani badala ya Saudi Arabia aalipotangaziwa donge nono.
Casemiro ambaye amezidi kuwa moto, hivi karibuni alikataa ofa mpya aliyotangaziwa Man United lakini wakati ikidhaniwa atakwenda Saudi Arabia, mwenyewe inadaiwa anataka kwenda kucheza na Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami.
Mmoja wa wamiliki wa Inter Miami ni nahodha wa zamani wa England na mchezaji wa timu za Man United na Real Madrid, David Beckham ambaye inadaiwa ndiye aliyesaidia kumshawishi Messi ajiunge na timu hiyo na sasa anatarajia kumshawishi Casemiro.
Casemiro hajaweka wazi atakwenda timu gani baada ya Man United lakini kinachojulikana ni kwamba mabilionea wa klabu za Al Nassr na Al Hilal za Saudi Arabia wamemtangazia mchezaji huyo ofa ili acheze soka katika Ligi Kuu Saudi Arabia au Saudi Pro League.
Kiungo huyo kutoka Brazil hata hivyo hayuko tayari kuihamishia familia yake Saudi Arabia badala yake angependa kwenda Marekani hasa katika klabu ya Inter Miami ambayo kwa ushawishi wa Beckham inaendelea kujiimarisha kwa kusajili wachezaji wa hadhi ya juu duniani.
Habari za ndani zinadai kuwa mabosi wa Inter Miami tayari wamemshawishi kiungo huyo kwa mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi mwaka 2028 na baada ya hapo wamemtengea ofa nyingine ya mwaka mmoja.
Casemiro licha ya kuwa na miaka 34, anaebdekea kuonesha kiwango bora kiasi cha kuwafanya mashabiki wa Man United kutaka kiungo huyo asiondoke lakini mpango wa klabu kubana matumizi ni sababu tosha ya kumfanya aondoke.
Katika mechi za karibuni za Man United, Casemiro amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu hiyo lakini mmoja wa wamiliki wa klabu, Sir Jim Ratcliffe yuko makini katika kupunguza gharama za mishahara ya wachezaji.
Casemiro analipwa Pauni 400,000 kwa wiki mshahara ambao hauendani na sera za kubana matumizi ambazo kwa sasa zinatekelezwa katika klabu hiyo kwa umakini mkubwa na Sir Jim Ratcliffe.
Kimataifa Casemiro akataa ofa ya Saudi Arabia
Casemiro akataa ofa ya Saudi Arabia
Read also
