Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Namungo, Mwinyi Zahera amesema wana kazi ya kufanya ili kuhakikisha wanapanda kwenye nafasi za juu za msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Zahera ameeleza hayo Jumatatu hii baada ya sare yao ya bao 1-1 katika mechi yao na Tabora United iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora akidai imevuruga mipango yake.
“Malengo yetu yalikuwa pointi tatu lakini vijana wangu walizembea kidogo, wapinzani wakasawazisha, sio mbaya tunajipanga kuhakikisha tunashinda mechi zijazo ili kurudi kwenye lengo letu kuu ambalo ni kupanda nafasi za juu,” alisema Zahera.
Zahera alisema ulikuwa mchezo muhimu kwake lakini hana namna zaidi ya kukubaliana na matokeo na kurudi uwanja wa mazoezi ili kupanga mikakati mipya itakayowapa ushindi wa mechi zinazofuata.
Kwa matokeo hayo Namungo FC, sasa imefikisha pointi 18 ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo katika mechi 15 ilizocheza.
Soka Zahera akiri Namungo kazi wanayo
Zahera akiri Namungo kazi wanayo
Read also