Madrid, Hispania
Nyota ya mchezaji mkongwe wa Real Madrid, Luca Modric imeanza kung’ara Jumamosi katika La Liga baada ya kupachika bao na kutoa pasi iliyozaa bao wakati timu hiyo ikiichapa Celta Vigo mabao 4-1.
Alikuwa ni mshambuliaji tishio wa timu hiyo, Karim Benzema aliyeandika bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 14 baada ya Renato Tapia kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Celta Vigo walisawazisha bao hilo dakika 10 baadaye nao wakifunga kwa mkwaju wa penalti iliyojazwa wavuni na Iago Aspas, penelti ambayo ilitolewa baada ya Eder Militão kuunawa mpira wakati akitaka kuokoa.
Baada ya hapo ndipo Modric alipoujaza mpira wavuni dakika ya 42 na kuipatia Madrid bao la pili kwa shuti la umbali wa mita 25 baada ya kuinasa pasi ya David Alaba na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko, Madrid ikiwa mbele.
Modric tena akamuunganishia Vinicius Jr pasi ya maana iliyozaa bao la tatu la Madrid katika dakika ya 56 wakati bao la nne la Madrid lilijazwa wavuni na Federico Valverde dakika 10 baadaye. Madrid wangeweza kuongeza bao jingine baada ya kupata penalti dakika tatu kabla ya mpira kumalizika lakini nyota wa zamani wa Chelsea, Eden Hazard alishindwa kuujaza mpira wavuni.
Modric, kiungo mkongwe mwenye umri wa miaka 36 sasa anakuwa amefikisha mabao 33 katika La Liga huku 18 kati ya hayo akiyafunga kwa mashuti ya nje ya 18, baadaye alijikuta akishangiliwa na mashabiki wakati akitoka kumpisha Dani Ceballos.
Kwa Madrid ushindi huo ni wa tatu mfululizo tangu kuanza kwa msimu wa 2022/23, ilianza kwa ushindi wa kwenye mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Eintracht Frankfurt na kufuatiwa na ushindi dhidi ya Almeria katika mechi yake ya kwanza ya La Liga. Matokeo ya mechi nyngine za La Liga ni kama ifuatavyo..
Celta Vigo 1-4 Real Madrid
Osasuna 2-0 Cádiz
Mallorca 1- 2 Real Betis
Kimataifa Mkongwe Modric afanya kweli
Mkongwe Modric afanya kweli
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
