Na mwandishi wetu
Mabondia 28 wanaounda timu ya taifa ya ngumi za ridhaa wameingia kambini wiki hii kujiandaa na mashindano mawili tofauti.
Mashindano ya kwanza ni ya All Afrika Games ambayo yamepangwa kufanyika nchini Ghana na mengine ni ya Olimpiki Paris nchini Ufaransa, ambayo yote yatafanyika mwaka huu.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa (BFT), Makore Mashaga (pichani) katika idadi hiyo, mabondia wanaume wapo 18 na wanawake 10 na kamati ya ufundi itakuwa na watu tisa.
“Timu imeanza mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani pale Mgulani JKT, shirikisho lipo katika mipango ya kuhakikisha linaendesha mashindano ya majaribio ya kimataifa mwishoni mwa mwezi huu (Januari) ili kupata mabondia watakaowakilisha taifa katika mashindano ya Afrika na kufuzu kushiriki Olimpiki,” alisema Mashaga.
Aliwataja mabondia wamaume na uzito wanaopigana kwenye mabano kuwa ni Abdulrazaq Hamisi (kg 48), Abdallah Mohamed (kg 51), Azizi Waziri (kg 54), Mwalami Salum (kg 57), John Dominick (kg 57), Hassani Mrutu (kg 60), Shaibu Jafari (kg 60), King Lucas (kg 63.5), Abdallah Mfaume (kg 67) na Elias Damson (kg 67).
Wengine ni Joseph Phillipo (kg 71), Alphonce Abel (kg 75), Ilankunda Daniel (kg 75), Yusuph Changalawe (kg 80), Mussa Wambura (kg 86), Matonyinga Kasala (kg 92), Mhina Richard (kg 92) na Alex Sita Mpini (kg 92).
Kwa upande wa wanawake ni Miriam Richard (kg 48), Seraphina James (kg 48), Umulkuruthum Mkumbi (kg 48), Zulfa Macho (kg 52), Aisha Iddi (kg 52), Latifa Said (kg 48), Vumilia Kalinga (kg 57), Leila Yazidu (kg 60), Beatrice Nyambega (kg 60) na Grace Joseph Mwakamele (kg 66).
Viongozi ni Samuel Kapungu, (kocha mkuu), Rogate Damiani (kocha msaidizi), Michael Changarawe, Hassani Mzonge, Kasim Husein na Maneno Omary (wote makocha), Maira Mussa (daktari), Makore Mashaga (meneja) na Ruger Kahwa (mlezi wa timu).
Ngumi Mabondia 28 waingia kambini
Mabondia 28 waingia kambini
Read also