London, England
Mshambuliaji Alexandre Lacazette ameondoka katika klabu ya Arsenal na kurudi klabu yake ya zamani ya Lyon akiwa mchezaji huru.
Kwa hatua hiyo, Lacazette anarudi katika klabu aliyoihama miaka mitano iliyopita na kujiunga na Arsenal kwa ada ya Pauni 46.5 milioni ambayo ilikuwa rekodi ya uhamisho katika klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 31, ameifungia Arsenal mabao 54 katika mechi 158 za Ligi Kuu England na kuisaidia kushinda taji la FA mwaka 2020.
Lacazette aliwahi kunukuliwa akisema kwamba katika maisha yake yote ameendelea kuwa na mawasiliano na Lyon ambayo ni klabu ya kwao na hivyo anafurahia kurudi katika klabu ambayo alijiunga nayo akiwa na miaka 12 huku ikidaiwa kwamba usajili wake ni jambo ambalo klabu hiyo imekuwa ikilipa kipaumbele kwa miezi kadhaa iliyopita.
Mchezaji huyo ambaye aliibukia timu ya watoto ya Lyon hadi kuweka rekodi ya kufunga mabao 129 katika mechi 275 kwenye mashindano yote tangu aingie kwenye kikosi cha wakubwa cha timu hiyo msimu wa 2009/10 kabla ya Arsene Wenger kumsajili katika klabu ya Arsenal mwaka 2017.
Lacazette alikuwa nahodha wa Arsenal baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka Arsenal na kutua Barcelona lakini Desemba mwaka jana kocha wa Arsenal, Arteta alimvua unahodha kwa kilichodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Kimataifa Lacazette aondoka Arsenal, arudi Lyon
Lacazette aondoka Arsenal, arudi Lyon
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
