Barcelona, Hispania
Nafasi ya mshambuliaji nyota wa PSG, Lionel Messi kurudi katika klabu yake ya zamani ya Barcelona inaonekana kuwa wazi baada ya watu wawili muhimu katika klabu hiyo kumzungumzia mchezaji huyo katika namna ya kumtaka arudi kumalizia soka lake Nou Camp.
Watu hao ni Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta ambaye wiki iliyopita alizungumzia uwezekano wa Messi kurudi katika klabu hiyo wakati mwingine ni kocha wa timu hiyo, Xavi Hernandez ambaye amesema milango haijafungwa kwa mchezaji huyo kurudi ‘nyumbani’ siku zijazo.
Katika suala hilo Xavi amekuwa wazi akisema kwamba kwa sasa nafasi ya kumsajili Messi kutoka PSG haipo kwa sababu Barca haiwezi kumudu gharama za kuingia mkataba na mchezaji huyo ambaye bado ana mwaka mmoja katika mkataba wake na vigogo hao wa Paris.
“Leo (Messi) ana mkataba hivyo haiwezekani, haina maana kwa sasa kumzungumzia, ndio ni mchezaji bora duniani, ni bora zaidi, rais tayari amemzungumzia akisema ana matumaini kwamba hadithi ya Messi na Barcelona haijafika ukomo, tutaangalia itakavyokuwa siku zijazo lakini huu si wakati wa kumzungumzia Messi, ni wakati wa kuwazungumzia wachezaji wazuri tulionao hapa,” alisema Xavi.
Baada ya Messi kuondoka, Barca imeendelea kujiimarisha ilisajili washambuliaji Robert Lewandowski na Raphinha hivi karibuni, kabla hapo, Januari iliwasajili, Ferran Torres na Pierre-Emerick Aubameyang.
Messi atafikisha miaka 36 wakati mkataba wake utakapofikia ukomo na PSG mwaka 2023, lakini amekuwa akihusishwa mno na mipango ya kurudi Barca.
Barca ililazimika kuchukua uamuzi mgumu kumruhusu Messi kuondoka katika klabu hiyo kwani licha ya kuwa tayari kupunguziwa mshahara lakini bado Barca wakajikuta katika wakati mgumu kumlipa mshahara wake ili kukidhi matakwa ya misharahara kwa mujibu wa kanuni za matumizi ya fedha kwenye La Liga.
Kimataifa Xavi: Messi anaweza kurudi Barca
Xavi: Messi anaweza kurudi Barca
Read also